“Home for Christmas”

Susan, mke na mama anabadilika na kuwa mraibu wa mihadarati. Anatoka nyumbani na kuwategemea wanaume ili akidhi haja zake za kupata dawa za kulevya na anasa za kila aina. Ni hadi wakati kwa Krismasi anapokumbuka kuhusu familia yake. Je, atapokelewa tena nyumbani? Ni katika flamu ya Home for Christmas, iliyotayarishwa na kuelekezwa na Linda Kinyita.

Baada ya kuitazama filamu hii, nimekuwa na hakikisho kwamba kuna tumaini katika uundaji wa filamu nchini Kenya. Kuna haja kubwa kuzinunua fiamu zinazotayarishwa nchini pasi na kuzitegemea nchi za nje kwa wanaozitazama filamu hizo nyumbani na hata vituo vya runinga.

Wapo wengi nchini wanavyo vipaji ila vimelala tu bila kazi yoyote. Tunapowaunga mkono waigizaji wetu, tutavikuza vipaji vyao na kuwawezesha kujikimu kimaisha kama biashara nyinginezo.

Kuchangia kwa maoni hakujawezeshwa.