(Android) Ushairi wa Mwanagenzi

Ushairi wa Mwanagenzi ni kitumizi cha Android kinachompa tumaini mshairi chipukizi aliye na ari ya kuwa malenga ili kuendeleza fani ya ushairi. Pamoja na kuimarisha washairi chipukizi. kitumizi hiki huelimisha na kuchanganua masuala tofauti yanayohitajika katika ushairi bora.

Utasoma mengi kutoka kwa washairi chipukizi nchini Kenya na Tanzania. Makala yametolewa kwa tovuti ya www.mwanagenzi.com iliyo na lengo la kuwapa moyo washairi chipukizi. Kuna maelezo kemkem yanayoelezea na kufafanua kuhusu ushairi wa Kiswahili. Ni maelezo na mashairi yatakayomfaa mwanafunzi wa shule ya msingi, sekondari au chuo kikuu.

Maelezo kuhusu Ushairi yatamfaa mtumiaji wa Ushairi wa Mwanagenzi. Licha ya kuwa na vitabu vilivyo na maelezo kuhusu Ushairi, watu wengi wamekuwa wakitumia wavuti jambo ambalo litawafaa sana vijana wa siku hizi wanaotaka kujua mengi kuhusu Ushairi. Ndipo hapa Mwanagenzi Mtafiti imezidua kitumizi kitakachowafaa wengi kujifunza Ushairi wa Kiswahili.Maelezo haya ni pamoja na Maana, Historia, Uainishaji na Uhakiki wa Mashairi.

Hivi hapa vidokezo vya kitumizi hiki:

  1. Mpangilio mwafaka wa maelezo kwa lugha teule ya Kiswahili.
  2. Mashairi yaliyopangwa kwa aina, washairi, maudhui na bahari.
  3. Arifiwa punde tu tunapochapisha mashairi mapya.
  4. Picha iliyoteuliwa kwa kila shairi inayoambatana na dhamira ya kila shairi.
  5. Soma shairi moja kwa jingine kwa urahisi wa kufungua.
  6. Hifadhi mashairi kwa kubonyeza kitufe ili uyasome baadaye.
  7. Shirikisha mashairi na makala kwa wengine kutumia Whatsapp, Facebook n.k.
  8. Linki muhimu zitakazokuelekeza kwa tovuti za Mwanagenzi Mtafiti.
  9. Tutazidi kusasisha kitumizi hiki na kuongeza maelezo, mashairi na makala mbalimbali ili kukufaa zaidi.

Tumia linki hii kupata kitumizi hiki – Ushairi wa Mwanagenzi

Kuchangia kwa maoni hakujawezeshwa.