Android: Jifunze Ushairi

Je wewe ni mshairi chipukizi ambaye ungependa kuinua tajiriba yako ya utunzi? Je ungependa kujiburudisha kwa maswali ya kusisimua ya chemsha bongo kuhusu ushairi? Ama una azimio la kufanya utafiti kuhusu ushairi wa Kiswahili? Tuna jawabu!

Jifunze Ushairi ni programu mpya ya Android kutoka kwa Mwanagenzi Mtafiti (www.mwanagenzi.com). Imeundwa kumsaidia mwanafunzi wa ushairi au mshairi chipukizi anayejifunza kutunga mashairi ya Kiswahili. Imeundwa kwa ufundi wa hali ya juu na inatumia Kiswahili kama lugha ya msingi.
Kando na vitabu vya ushairi, ni bora kutafuta njia mbadala zinazoelezea kwa kina kuhusu ushairi. Hivyo basi, Mwanagenzi Mtafiti imefanya utafiti na kuzindua programu hii itakayomfaa yeyote aliye na ari ya kujifunza ushairi.

Vidokezo:

 1. Soma makala mbalimbali kuhusu Ushairi; Dhana, Uainishaji, Uhakiki na mifano ya mashairi.
 2. Elekezwa kutunga mashairi hatua kwa hatua ukisoma nguzo muhimu katika utunzi wa mashairi.
 3. Mpangilio aali wa programu unaopendeza.
 4. Jiburudishe kwa mchezo wa kujibu maswali ya Ushairi.
 5. Pata Alama zako na majibu ya maswali yote uliyoyajibu.
 6. Hifadhi makala ili iwe rahisi kuyapata na kuyasoma baadaye.
 7. Pokea arifa punde tu tunapochapisha makala mapya.
 8. Badilisha ukubwa wa fonti ili ukufae kusoma unavyopenda.
 9. Shirikisha rafiki kwa kumtumia baadhi ya maelezo.
 10. Hakuna matangazo yoyote ya biashara.
 11. Utasoma makala yote bila kuwa hewani kwa mtandao.

Kuchangia kwa maoni hakujawezeshwa.