Mwandishi: Kimani wa Mbogo

Mahinda Matano

Mahinda Matano

Alikuwa mcheshi na mtoto aliyependa mbwembwe za kila aina. Mwalimu wake alimpenda na alijizatiti kuzibadilisha tabia zake zilizoathiri hali yake ya masomo. Mahinda Matano ni mtoto wa shule, mtundu na asiyesikia la mwadhini wala la mteka maji msikitini. Anapokuwa darasani huwatumbuiza wanafunzi wenzake. Akiwa nyumbani hufanya vituko na sarakasi ambazo huwaudhi wazazi wake.  Hadithi inakamilika …

Soma Zaidi Mahinda Matano

“Tenda Wema Nenda Zako”

“Tenda Wema Nenda Zako”

Kila anapoamka, mja huwa na tumaini la kutarazaki kwa fanaka na hatimaye kupata fedha atakazozitumia kugharamia mahitaji yake ya kila siku. Hujitolea kwa uwezo wake wote kung’ang’ana angalau apate lishe bora, mavazi na pahali pa kuishi. Hata hivyo, mengineyo huwa ni bahati yake. Mwanadamu anapofanikiwa husahau mateso aliyoyapitia. Wengine huwapata marafiki wengine wanaowiana kwa hadhi …

Soma Zaidi “Tenda Wema Nenda Zako”

Umaarufu wa Shaaban Robert

Umaarufu wa Shaaban Robert

Kila linapotajwa jina lake, dhana ya ubingwa inayohusu lugha ya Kiswahili hutanda mawazoni. Shaaban Robert alichangia kwa mengi ambayo hata sasa yangali yanakumbukwa na wengine kuenzi maisha yake. Shaaban anakumbukwa kama bingwa aliyechangia katika lugha ya Kiswahili kwa kazi zake za fasihi, ambazo kufikia sasa, asilimia kubwa imekusanywa na kuchapishwa kwenye vitabu mbalimbali. Baadhi ya …

Soma Zaidi Umaarufu wa Shaaban Robert

Anayeumia ni Mpiga Kura

Anayeumia ni Mpiga Kura

Tunapopiga kura si kwamba tu tunafanya zoezi la kidemokrasia bali ni kuchagua viongozi wema watakaotuwakilisha vilivyo. Isiwe ni jambo la mazoea kuamka mapema siku hiyo ili uwapiku wengine kwenye safu ndefu za Wakenya wengine wazalendo. Licha ya wanasiasa kuwarai wapiga kura kutekeleza wajibu wao inapaswa pia ifahamike wazi umuhimu wa kupiga kura. Wengi wetu wamefanya …

Soma Zaidi Anayeumia ni Mpiga Kura

Ujana Haudumu

Ujana Haudumu

Leo tarehe 06/03/2017 ilikuwa siku ya buriani kwa Gavana wa kwanza jimbo la Nyeri, Nderitu Gachagua. Licha ya shughuli nyingi, niliamua kuwa na wakati ili kufuata yaliyojiri wakati wa tukio hilo la kumuaga Gavana. Yalikuwa mazishi ya kwanza kwa mtu wa cheo hicho hapa nchini Kenya chini ya katiba mpya iliyozinduliwa mwaka wa 2010. Wengi …

Soma Zaidi Ujana Haudumu

Jamii ya Kizazi Kipya

Jamii ya Kizazi Kipya

Najihurumia kuwa katika jamii iliyojaa misukosuko ya kisiasa, ukabila na majanga tofauti. Hili ni jambo ambalo limeniumiza moyo sana na kunipa mshawashawa kuandika makala haya. Haifani unapoishi katika jamii iliyojaa waasi, wahuni na waroho. Huenda ikawa ni shinikizo watu wa maeneo haya wanyoyapata kutoka kwa viongozi wao. Uvivu ni mojawapo ya mambo yanayoathiri taswira ya …

Soma Zaidi Jamii ya Kizazi Kipya